UNYAMA WA MAMA MZAZI

VITENDO VYA UTESAJI, UNYANYASAJI VYASHITUA BUSEGA

AFUNGWA KAMBA MIGUU, MIKONO NA SHINGONI

Na Shushu Joel, Busega


WANANCHI  wilayani  Busega mkoani Simiyu katika  kata ya kabita kijiji cha nyakaboja wamekasilishwa na ukatili na unyanyasaji uliofanywa na Nyafulu (Neema) Makoba  ambaye ni mama mzazi wa Sikolastica Paul  mkazi wa kijiji cha nyakaboja  wilayani busega.

Mariam Joans ni jirani wa mama huyo anaeleza kuwa ni kawaida yake Neema Makoba kumtesa mototo huyo kwani mara nyingi tumekuwa tukisikia sauti ya motto huyo akiwa analia toka ndani, Mimi na mmewangu tulijaribu kumkanya lakini alishindwa kabisa kutuelewa


Jana majira ya saa 1 asubui nilisikia kelele ya motto Scolastika akilia kwa sauti ya juu sana na ndipo nilimwamuru mume wangu twende tukamsaidie mtoto huyo mara baada ya kufungua mlango tulimkuta amefungwa na kamba miguuni,mikononi na shingoni na kasha kamba hiyo kufungwa kwenye nondo za dirishani.   

Kutokana na hali hiyo kuiona mme wangu alimkimbilia mtendaji wa kijiji Mariam Kagusa naye alipofika alimuona motto huyo akiwa katika hali hiyo huku mda huo mama mzazi wa binti huyo hakuwepo nyumbani kwake. 
Mtendaji wa kijiji aliwaamuru wananchi kuweza kumchukua mtoto na kumpeleka kwa Afisa ustawi wa jamii wa Busega Grace Mmasi naye kuamuru mama huyo aweze kupelekwa katika kituo cha polisi.

Afisa ustawi huyo alisema kuwa ni kitendo cha kinyama kwa mama huyo kuweza kumfanyia mtoto huyo asiyejua kitu chochote masikini. 
Mara baada ya kuhojiwa na mwandishi wa NIPASHE mama huyo alisema kuwa alimpatia adhabu hiyo scolastika kutokana na kupotea kwa kiasi cha shilingi elfu tano ndani.

Kwa upande wake binti Scolastica Paul anasema kuwa si kweli yeye hakuchukua pesa hiyo kwani mama ni muongo na ni mda mrefu amekuwa akinitesa na kuninyima chakula na hata kunifungia kwa nje na yeye kuweza kwenda kuangalia video katika mabanda.

Aliongeza kuwa ndani mwao kulikuwa na kiaasi cha shilingi mia mbili mbili yaani 400 sasa sijui ni kwa nini mama anashindwa kusema ukweli juu ya hili, kwani hata shule kashindwa kunipeleka wakati babu alimpatia pesa ya mahitaji yote.


Alipofika Babu na mjomba wa mtoto huyo walimchukua na kuondoka naye huku baba mzazi wa neema akisema kuwa anaiomba mahakama kuweza kutoa fundisho kwa bintiyake kwani ni muuaji na pia aliweza kumchukua mjukuu wake na kuahidi kumpeleka shule.

Polisi wilayani Busega inakamilisha hatua za kisheria ili iweze kumfikisha mahakamani.



Comments