Sehemu ya Kwanza
Na Aloyce Kalunde
Neno ndoa linatafsiri mbalimbali
kulingana na mila ya mahali fulani. Lakini kwa ujumla ni muungano halali wa
kijamii, kisheria wa watu wawili wa jinsia tofauti, mume na mke walio amua
kuishi pamoja kwa hiari yao ili kutimiza kusudi la Mungu. Huu ni uhusiano wa
ndani sana unaohusisha urafiki na tendo la ndoa.
KWA
NINI KUOA/KUOLEWA?
Katika mazingira tofauti tofauti watu huoa
au huolewa kwa sababu mbalimbali kama za kijamii, kisheria, kupendana, kujamiiana,
kihisia, kiuchumi, kiroho na kidini. Lakini jambo moja kuu ni kuwaleta pamoja
watu wawili waliotofauti ili hatimaye waweze kushirikiana kwa pamoja mali zao
na pia uwezo na vipaji vyao katika maisha. Wanaingia katika hali ya kushirikiana
hali zote za maisha, njema au mbaya, furaha na huzuni, hofu, mafanikio nk.
Mahali pengi duniani na hasa Afrika,
kupata watoto katika ndoa huwa ni jambo linalochukua umuhimu mkubwa katika ndoa.
Katika mazingira kama haya ndoa haiitwi imekamilika bila kuwa na watoto.
Hutokea mahali pengine wanaume kuoa mke mwingine endapo mke wa kwanza hana
uwezo wa kuzaa mtoto. Ikumbukwe kwamba katika Biblia ndoa zilikuwepo zenye
watoto na zisizo na watoto. Hivyo dhana hiyo siyo sahihi kwamba ndoa bila
watoto siyo ndoa, Biblia haisemi kitu cha namna hiyo.
Muungano huu wa watu wawili hukamilishwa
kwa tendo la ndoa ikiwa ni njia ya kuimarisha uhusiano wao kwa namna ya kipekee
sana kiasi kwamba hujisikia kuwa mwili mmoja.
Mungu alipomuumba Eva (Hawa) na kummpa Adamu alitaka wawe na ushirika na kila
mmoja kumtambua mwenziwe na kutegemeana na kumtegemea Mungu. Ushirika wao huu
ungekamilishwa kwa tendo la ndoa. Tutaangalia kwa undani habari hizi katika
somo husika. Sababu zingine za watu kuoa au kuolewa ni:
Ni
tiba ya upweke
Watu huoa na kuolewa ili kuondoa upweke.
Adamu alipokuwa peke yake alikuwa na huzuni na upweke. Lakini alipokuja Hawa
upweke uliondoka kwa vile alimpata mwenzi wake ambaye hakupatikana miongoni mwa
wannyama ambao aliishia kuwapa majina tu na siyo kupata ushirika wowote
(Mw.2:18).
Huleta
furaha na raha
Watu huamua kuishi pamoja ili kupata
furaha na raha. Mfalme Abimeleki alitambua kuwa Isaka na Rebeka walikuwa ni mtu
na mkewe alipowaona wakicheza chumbani wakifurahiana.
Kutuepusha
na tamaa na uzinzi
Paulo anasema kila mtu na awe na mke
wake mwenyewe ili aweze kupata raha ya tendo la ndoa kwa mke wake wa ndoa na si
vinginevyo. (1Kor.7:2).
Ili
kukamilishwa na mwenzi wake wa ndoa
Mwanaume ana pengo ambalo linatakiwa
kujazwa na mkewe na kwa mwanamke vivyo hivyo. Kilammoja hajakamilika bila
mwenzi wake wa maisha (Mwa. 2:21-22); Mat. 19:3-6). “Adamu peke yake alikuwa
hajakamilika , alikosa mwenzi wa kumfanania mpaka alipoumbwa Hawa.”
Ndoa
huleta heshima katika jamii
Watu wanaoana ili kupata heshima katika
jamii, kwani mtu aliyeoa au kuolewa ana heshima ya tofauti na yule ambaye
hajaoa au kuolewa.
Ndoa
huleta usalama na ulinzi kwa wanandoa
Kuoa na kuolewa katika jamii ni ulinzi. Kuna kuogopwa
kwa wanandoa katika jamii husika (Yer.31:22; 1Kor.7:37).
Ili
kuendeleza uumbaji wa Mungu kwa kuzaliana
Mungu anapenda tuwe na familia na watoto
ambao ni baraka kutoka kwa Mungu (Mwa.1:28).
MAMBO YANAYOHARIBU NDOA
Kuna mambo yanayoweza kuharibu ndoa yako
kama hutakuwa makini. Kuna sababu kadha wa kadha zinazochangia kuvunjika kwa
ndoa:
Kukosauaminifu
katika ndoa.
Baadhi ya wanawake na wanaume (wanandoa)
huanza kuwa na wanaume au wanawake wa pembeni, hili ni kosa kubwa katika mpango
wa ndoa aliouanzisha Mungu.
Kutokumpenda
mwenzi wako wa ndoa.
Kuwapenda watu wengine kuliko mwenzi
wako wa ndoa hupelekea kuvunjika kwa ndoa. Ikitokea mume anawapenda rafiki zake
au jamaa yake kuliko mkewe, na vivyo hivyo mwanamke, ndoa hiyo huwa iko
hatarini kuvunjika.
Kukosekana
kwa mawasiliano mazuri.
Hali hii huleta kutokuelewana kwa
wanandoa, yaani kila mmoja kuwa mbinafsi na kujali matakwa yake tu. Mawsiliano
huweza kuharibiwa na:
Ø
Matakwa
binafsi.
Ø
Kutokuwa
wazi baiana ya wanandoa.
Ø
Kupuuzia
mambo.
Ø
Kutopeana
nafasi ya kusema na kusikilizana baina ya wanandoa.
Ø
Kuskiliza
zaidi kitu cha nje na kuamini kuliko anachokuambia mwenzio.
Kutokuwa
na mipaka katika ndoa.
Watumishi wanyumbani, mawifi, mama mkwe wa
pande zote ni lazima wawekewe mipaka katika ndoa. Kwa kuwa ndoa ni ya watu
wawili, mtu wa tatu ni ibilisi.
Kutokuwa
na umoja.
Kukosekana kwa umoja au ushirika kwa
wanandoa hufungua mlango wa ndoa kuvunjika. Hii ni pamoja na kuwa na ubinafsi
na kulimbikiza vitu moyoni kwa kukosa roho ya msamaha baina yao.
Kuyumba
kwa uchumi.
Uchumi unapoyumba huweza kutokea
kutokuelewana kwa wanandoa kwa sababu ya kukosekana kwa mahitaji mbalimbali
nyumbani.
Ugumba
au utasa.
Hali hizi huondoa amani katika ndoa na
kusababisha hata kuvunjika kwa ndoa nyingi.
Shida
za mateso.
Ugomvi, shida, manyanyaso, vitu hivi
vikiwepo mara kwa mara huweza kupelekea ndoa kuvunjika.
Kutokuomba.
Kutoombea ndoa huweza kumpa Ibilisi
nafasi ya kuivuruga na kuivunja (Sam. 12:23).
Kunyimana
unyumba.
Kumnyima mwenzi wako wa halali tendo la ndoa
kunaweza kutoa mwanya kwa mwenzi wako kumtafuta mwingine atakayemridhisha na
kumfurahisha katika tendo hilo. Hasara za kunyimana tendo la ndoa:
Ø
Ugomvi
mkubwa hutokea baina ya wanandoa.
Ø
Kutoka
nje ya ndoa.
Ø
Kutopendana
na kuchukiana.
Ø
Kutoheshimiana.
Ø
Kiburi
na kutoelewana.
Ø
Kuvunjika
kabisa kwa ndoa
Kutoaminiana.
Hapa ni chanzo cha kuharibu ndoa,
kwamaana imani inakosekana pande zote mbili.
Kukaa
muda mrefu mbalina kumwacha mwenzi wako wa ndoa.
Hali hii huweza kufungua mlango wa
uzinzi kwa wanandoa wengi na hivyo kusababisha kuvunjika kwa ndoa.
Kukosa
uvumilivu.
Kushindwa kuvumiliana katika mambo
mbalimbali yanajitokeza katika ndoa kwa mwenzi wako. Hii ni sababu moja wapo ya
kuvunjika kwandoa.
Kukosa
muda wa kukaa pamoja na familia yako.
Kutopeana nafasina mwenzi wako ya
kuongea na familia hujisikia kama hathaminiwi, na hivyo kuvuruga ndoa.
Tuma maoni yako kwa:
+255 783700083
+255 653 700083
Comments
Post a Comment