WAATHIRIKA WA UKIMWI WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA.


Na Shushu Joel, Busega.
0782 466366
Kikundi cha watu wanaoishi na maambukizi ya ugongwa wa ukimwi toka katika wilaya ya busega mkoa wa simiyu wametoa ombi lao kwa serikali ya Tanania kwa niaba ya wenzao wote walio na ugonjwa huo na tayari wamejiunga katika matumizi ya ARV.

        wathibiti wa maambukizo ya ukimwi wilayani busega pia ni waathirika wa ugonjwa huo.

Kikundi hicho chenye jin la kamati ya kuthibiti maambukizi ya ukimwi wilayani busega (SIMAKI) chenye wanachama wasiopungua 50 kimetoa lalamiko kwa serikali kwa kutokupatikana kwa dawa za kupunguza makali kwa waathiria  katka siku ya ukimwi nchini.

Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti walisema kuwa kwa sasa kumekuwa na uhaba mkubwa sana katika kupewa kwa dawa hizi ukilinganisha na miaka ya nyuma mgonjwa alikuwa anapewa dawa za kumeza za mwezi mzima lakini kwa sasa hivi imekuwa sivyo kwani tunapewa dawa za kumaliza wiki moja hivyo hali hii sisi inatuumiza sana ukilinganisha na pato letu.

Bwana Nandi Bulengera yeye ni mjumbe katika kamati hii anasema kuwa wanakumbana na changamoto nyingi sana katika jamii inaowazuguka ikiwemo ya kubaguliwa, kutothaminiwa lakini yeye anaona hali hii ni ya kawaida kwake na anahitaka serikali kuweza kuwawezesha wagonjwa hata wa kuwapa matunda kwa kila mwisho wa mwezi ili afya zao ziweze kuwa fiti zaidi.

Bi Penina Palapala yeye alianza kutumia ARV mwaka 2006 mpaka sasa anaendelea vizuri sema analalamikia kwa watu kuona aibu kupima afya zao ili waweze kujitambua kama wanamaambukizi au vp, Hivyo B I penina ameitaka serikali kuendelea kutoa nafasi na kipaumbele kwa watu walio na maambukizi ya ukimwi hapa nchini kwa kuwapa dawa za kutosha na hata kutoa vyakula kwa wale wasiojiweza kwani dawa hizi zinanguvu sana hivyo inahitaji kupata lishe bora.
Pia mwanachama mwingine ni Sospiter Majige anaeleza kuwa alianza kutumia dawa za ARV mwaka 2007, Hivyo aliitaka serikali kuweza kuongeza juhudi za kuongeza uwepo wa vituo vingi vya utoaji huduma kwa watu wenye maambukizi ya ukimwi.

        Wajumbe wanaoamasisha watu kupima ukimwi kwa hiari wilayani Busega na 
        wao pia ni waathirika wa ugonjwa huo.
Upande wa serikali iliwakilishwa na  makamu mwenyekiti wa halmashaul ya busega Bw, Mngumbi Mojo anasema kuwa anaishukuru sana kamati ya kuthibiti maambukizi ya ukimwi wilayani busega kwa utendaji mzuri wa kazi zao kwa kuhamasisha watu kupima na kutambua afya zao .

Mojo aliongeza kuwa tatizo bado lipo kwa wakazi wanaoishi kando kando mwa ziwa (mwaloni) hawa ndiyo chanzo cha maambukizi ya maradhi katika wilaya yetu hivyo basi aliitaka serikali kuweza kuongeza juhudi binafsi ili kuweza kupambana nawatu hawa.
Tanzania mpya bila maambukizi ya ukimwi inawezekana ndiyo kauli ya makamu mwenyekiti huyo.

Comments