Na Shushu
joel
Busega,
Simiyu
Shirika la
mfuko wa hifadhi ya jamii nchini (NSSF) wameamua kujitosa ili kuweza kupambana
na kero zot za wavuvi nchini bila kubagua wala upendeleo wowote ule .
Hya
yamesemwa leo katika kijiji cha Ihale kata ya kiloleli wilayani Busega mkoani
simiyu na Meneja wa Nssf mkoa wa shinyanga na simiyu Bw, James Mashinga wakati akitoa semina kwa wavuvi wa eneo hilo.
Mashinga
aliwata wakazi hao wa Ihale waweze kutumia fursa hii ya pekee ambayo imeamuliwa
kutolewa na shirika hilo pekee nah ii imetokana na shirika hilo kuona
wavuvi,Wakulima na Wafugaji kusahaulika na serikali.
Alisema kuwa
watakao jiunga na shirika hili watapata huduma nyingi bure ikiwemo matibabu ya
hospital kwa familia yaani Baba, Mama na watoto wasiopungua wanane pia
kutokuwepo na fursa za kupewa mikopo ya kipekee kwa wanachama ili waweze
kuondokana na masuala ya kuajiliwa na waweze kujiajiri wao wenyewe.
Aidha
Mashinga aliwasihii sana wana Ihale kuweza kutumia nafasi hii ya kipekee kwao,
hivyo aliwaambia mara baada ya kumalizana na wavuvi watahamia katika sekta
nyingine na lengo likiwa ni kuwakwamua katika janga la umasikini.
Kwa upande
wake Afisa uvuvi wa wilaya hiyo ya busega Bi Judith Mgaya ameweza kutoa wito
kwa wavuvi kuweza kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata huduma ya hifadhi ya
mfuko wa jamii kwani ni fursa ya pekee kwao kuweza kujikwamua katika hali ya
uchumi hapa nchi pia Bi mgaya aliweza kutoa pongezi kwa shirika la Nssf kwa
kutambua shida za wavuvi nchini na kuweza kupambana nazo.
Upande wa
wananchi wa Ihali waliojitokeza kwa wingi kuweza kujiunga na huduma hizo za
kijamii wakisemewa na Bw, Dionis Kabati anasema kuwa wao kama wavuvi
wanaishukuru Nssf kwa kuweza kutambua kero zao na hata kupata elimu ya kuwa kuna
mambo kama hayo ambayo sisi tulikuwa atuyajui kabisa, Hivyo aliwata viongozi
hao wa Nssf kuwa nao karibu zaidi ili waweze kubadilisha maisha yao.
Mwenyekiti
wa BMU katika mwalo wa Ihale Bw, Pius mazima anasema kuwa sasa ni wakati
mwafaka wa wavuvi kujikwamua na kwa hili hata uvuvi harama utakuwa kikomo
nchini.
Inafurahisha kutupata habari za mkoa wa Simiyu na wilaya zake. Tunaomba ututambulishe wahusika tupate kuwajua.
ReplyDelete