TALGWU  KUGOMEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA,VITONGOJI NA ULE MKUU WA MWAKA 2015.

Na Shushu Joel
Busega, Simiyu




Mpango kabambe unaoandaliwa na Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini kimeandaa mipango kabambe ya kugomea kutokushiriki kusimamia wala kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hapa nchini tarehe 14?12/2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Akifafanua sababu za kugomea uchaguzi huo kaimu katibu mkuu wa Talgwu hapa nchini Bw,njaa Kibwana  ni kuitaka serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kukilipa chama chao deni lao la kiasi cha shilingi billion 18.

Akizungumza na wanachama wa TALGWU wilayani busega Kibwana aliwataka wanachama hao kuwa na umoja ili waweze kufanikisha kulipwa kwa deni lao toka serikali npia nao kuweza kuthaminiwa kama vyama vingine vinavyopata thamani hapa nchini.
Aidha Kibwana alisisitiza kuwa wanachama sasa inatubidi kuwa wajasiri katika kudai masilahi yetu sisi wanachama na mwaka huu itabidi tuonyeshe mfano wa kuwa nasi tunaumuhimu katika serikali sasa tunaelekea kugomea chaguzi zote mpaka tulipwe madeni yetu alisema naibu katibu mkuu wa huyo hapa nchini.

Kwa upande wao wanachama waliohudhulia katika kikao hicho cha naibu katika mkuu cha kuwataka wanachama wake kugomea uchaguzi, katibu wa TALGWU wilaya ya busega mkoani simiyu Bw, Daniel Zacharia amesema kuwa wao kama wanachama wako tayari kwa hilo kwani wao ndiyo watendaji wakuu katika chaguzi mbalimbali hapa nchini , Hivyo wanaiomba serikali kuweza kulipa deni lao ndipo watashiriki katika chaguzi hizo.

Wanachama wa TALGWU wilayani busega wakiongozwa na Mathias Kahema anasema kuwa wanakiombasana chama chao kuwa na umoja, ushirikiano na ujasiri ili waweze kufikia malengo yao na pia aliutaka uongozi wa TALGWU hapa nchini kuweza kuweza kuwa karibu zaidi na wanachama ili kuweza kutatua kero za watumishi hao kwani wanakero nyingi sana zinazowakabiri .
Pia aliongeza kuwa maia ya kero zinazotusumbua ni kutothaminiwa na serikali yetu hivyo sasa hiki ni kipindi chetu kuonyesha nasi tupo na tunaumuhimu kiasi gani nchini cha msingi ni umoja na ushirikiano.   

Comments