Na Shushu joel
Busega
Gari lenye namba T 714
BJB aina ya scania lifanyalo safari zake toka msoma kwenda Mwanza
limeacha njia na kuingia darajani katika kijiji cha masanza kona kata ya kiloleli
wilayani busega katika mkoa wa simiyu.
Chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa taili ya mbele ya
kulia na hivyo kufanya gari hilo kuingia darajani na huku ndani ya daraja hilo
kulikuwa na maji mengi hivyo gari hilo kuingiliwa na maji pia.
Dereva wa gari hilo Bw, Edward Juma anasema kuwa alijaribu kujitaidi ili
kulizuia gari hilo kuingia katika mto huo lakini ilinishinda hivyo ilinibidi
niiweke tu ndani yam to huo, gari ilikuwa na abilia 60 na wala hakuna mtu hata
mmoja aliyepoteza maisha na hata majerui ni yale ya kawaida,
Mery Mwita ni abilia aliyekuwa anatoka msoma kwenda mwanza
anaeleza kuwa anampongeza sana dereva wa gari kwa ujasili wake wa kulifanya
gari hilo kutokuanguka na kuweza kuokoa maisha yetu sisi abilia wake.
Pia Franciss mongela anasema kuwa kama dereva asingekuwa
makini basi leo tungesema mengine hivyo mungu ambaliki huyu kijana .
Katika gari hilo pia kulikuwemo na askali polisi Bw, Joseph Christopher
mwenye namba H 812 PC kutoka kituo cha busega aliyekuwa akipeleka maabusu
wilayani magu mkoani mwanza yeye anaeleza kuwa gari lilikuwa katika mwendo wa
kawaida sema ajali ni ajali hivyo cha msingi ni kumpongeza dereva kwa kazi
nzuri aliyoionyesha mbele ya abilia wake.
Comments
Post a Comment