WANANCHI
WAGAWANA NYAMA YA FISI BUSEGA.
Na shushu joel
Busega, simiyu
Wakazi wa kitongoji cha mwamsikula A kijiji cha Bukabile kata
ya kabita wilayani Busega na katika mkoa wa Simiyu jana walitoa ya kufunga
mwaka 2014.
Wakazi hao walimkuta
fisi huyo amedumbukia kwenye shimo la choo katika nyumba ya mzee Finias Udoe
nyakati za usiku na hivyo wananchi hao kuweza kumtoa fisi huyo ndani ya shimo
hilo majira ya saa 3 asubui na kisha
kuweza kumgawana nyama yake.
Wakizugumza kwa wakati tofauti wakazi hao wanasema juu ya
matumizi ya nyama yamnyama huyo.
John Okuku ambaye pia
ni mweyekiti wa kijiji cha Bulima anasema kuwa wananchi hao waligawana mnyama
huyo kwa imani za kishirikina zilizowatawala katika nafsi zao
Mwenyekiti huyo aliwataja waliogawana nyama hiyo kuwa ni
Magesa mkwaja aliyechukua sehemu za siri za mnyama huyo, Mganga mmoja wa
kienyeji toka wilayani Bariadi amabaye pia ni kiongozi wa sungusungu katika
wilaya hiyo aliyejulikana kwa jina laNyakali Goloneli kwa upande wake alichua
kiganja cha mkona wa kushoto na kusema kuwa hii ni dawa ambayo inatibu magonjwa
mengi katika mwili wa mwanadamu.
Kwa upande wake mwenye nyumba ambako fisi huyo alidumbukia
Bw, Finias Mdoe anasema kuwa siku ya tukio yeye alikuwa amelala kwa watoto wake
jirani na kwake ambapo asubuhi alikuta tukio la namna hiyo nyumbani kwake
lakini mzee huyo alisema kuwa hata yeye anashangazwa na kitendo cha wananchi
hao kugawana mnyama huyo
Pia mzee huyo alikwenda mbali zaidi baada ya kusema kuwa fisi
huyu alikuwa amekatwa masikio kama vile tunavyokata wanyama wetu wa kufuga kama
mbuzi na kondoo nah ii ikiwa na maana kuwa ni alama yako wewe mfugaji sasa kwa
fisi huyu sijui labda ni alama ya mwenyewe.
Mpaka wananchi hao wanamaliza kugawana mnyama huyo hakuna mtu
yeyote Yule kutoka mamlaka ya wanyama poli aliyefika katika tukio hilo la
kusikitisha la kugawana kwa nyama ya fisi.
Comments
Post a Comment